Njia Rahisi Ya Kuchukua Namba Kutoka Kwa Mwanamke Unayemjua - NYUMBA YA MAPENZI

Breaking

Sunday, January 27, 2019

Njia Rahisi Ya Kuchukua Namba Kutoka Kwa Mwanamke Unayemjua

Kuchukua namba kutoka kwa mwanamke ni rahisi zaidi kuliko hata kutamka jina lako. Unachohitajika ni kuenda moja kwa moja kwa mwanamke unayetaka kumuomba namba halafu unamwagiza akupatie. Mara nyingi mwanamke hawezi kukataa kukupatia namba yake unless uwe umemuapproach kwa njia isiyofaa ama hakujui.

Mara ya mwisho mimi binafsi nilichukua namba kwa mwanamke chini ya dakika moja ya kukutana na yeye. Nilikuwa nimeandamana na marafiki zangu halafu mwanamke mmoja akapita kando yetu halafu muda wa dakika nikaamua kumuaproach na kunipatia namba yake ya simu hapo hapo.
Kama bado unatatizika ni njia gani za kuchukua namba ya simu kutoka kwa mwanamke basi fuata maagizo haya ya haraka ambayo nitakuelezea.

#1 Jiamini. Kujiamini ni kitu muhimu. Wakati unapoamua kuapproach mwanamke lazima uwe unajiamini. Utajiamini vipi? Kujiamini ni rahisi. Kile unachohitajika kufanya ni kuweka nia kuwa wakati ambapo utamwaproach mwanamke lengwa basi lazima namba yake ya simu atakupatia. Huko ndiko nikujiamini.

#2 Kuwa na mawazo chanya. Mawazo chanya ni mawazo ambayo yanakubaliana na wewe. Mfano unaweza kuwa unataka kufanya kitu, halafu katika akili yako umeweka dhana ya kuwa kile ambacho unakusudia kufanya basi kitafanikiwa. Haya ndio tunayaita mawazo chanya. Ni dhana ambayo unaamini kuwa itatokezea. Ukiweka mawazo chanya kuwa ukiapproach mwanamke flani na atakupa namba yake ya simu basi bila shaka utafanikiwa. Lakini ukiweka mawazo ya kuwa hautafanikiwa basi kweli hautafanikiwa.

#3 Kuwa mwigo. Wakati mwingine inakuwa vigumu kabisa kwa wanaume flani kuongea na mwanamke. Inakuwa vigumu zaidi kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Njia rahisi ya kutatua shida hii haraka ni kuigiza. Kuomba mwanamke namba haichukui zaidi ya dakika mbili, hivyo unaweza kuwa mwigo. Unaweza kuigiza vile rafiki yako anavyoomba namba ya simu ama unaweza kufanya mazoezi kivyako kabla kumuapproach mwanamke kumuomba namba ya simu.

#4  Relax. Wakati unapoach mwanamke lazima uwe umetulia. Punguza wasiwasi, toa kijasho chochote ambacho uko nacho, pumua kiutulivu na uondoe ubabaifu wowote ulio nao. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa umerelax utakuwa na nafasi nzuri ya kukumbuka mambo ambayo umeyapanga kumwambia mwanamke flani. Hivyo ni muhimu kurelax kabla ya kuchukua approach yeyote.

No comments:

Post a Comment