Marafiki
zangu kukosea katika maisha ya binadamu ni kawaida. Ni sehemu ya maisha
yake. Tena inaaminika kwamba, kukosea ni kujifunza, maana kosa
utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika uhusiano na
wapenzi wetu, mara kadha wa kadha tumejikwaa na kuwakosea.
Hakuna
cha ajabu. Ni kawaida kabisa, lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna
gani tunajifunza kupitia makosa. Ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti
hizo. Maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe,
lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku.
Lakini pia, wapo ambao kwa bahati mbaya, bila matarajio yao, wanajikuta wakiwa wamewaudhi wapenzi wao. Ni bahati mbaya na yawezekana kabisa wanaumia sana mioyoni mwao, lakini wakashindwa jinsi ya kumaliza ‘bifu’ hilo katika penzi lake.
Siku zote mkosewa hukosa raha, hupoteza hamu ya kukutana na mpenzi wake lakini kubwa zaidi, hujishusha/hukushusha thamani ya mapenzi yake kwako. Lakini mkosewa huyo huyo, akioneshwa kwamba makosa yaliyofanyika hayakuwa ya makusudi na kutumia njia bora za kufikisha hisia zako kwake, hujisikia amani na hali yake kurejea kawaida.
Rafiki zangu, yawezekana ukawa upo katika kipindi cha matatizo na mpenzi wako na hujui jinsi ya kuweka mambo sawa. Wakati mwingine huna tatizo, lakini kwasababu upo kwenye uhusiano basi si ajabu mambo kwenda mrama siku moja.
Hapa chini, nimekuandalia mambo matano muhimu ya kuzingatia unapokuwa umekwenda kinyume kidogo kwa mpenzi wako. Weka ubongo wako wazi, kuruhusu somo hili kichwani mwako, ambalo litakuwa hazina yako na mwongozo katika uhusiano wako.
KOSA LINA UKUBWA GANI?
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwasababu hujamwambia chochote, naye hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.
Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?
Mathalani unaweza kuwa ulimuudhi kwasababu alikupigia simu zaidi ya mara kumi bila kupokea, akakasirika. Hili ni kosa dogo.
Lakini yawezekana alikuta.

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments:
Post a Comment