Kuna
baashi ya wanaume wanatamani wakati wakiwa wanafanya mapenzi na wenzi
au wapenzi wao basi mboo zao ziwe zinasimama muda mrefu mathalani masaa
matatu au manne au zaidi huku wakimwaga shahawa eti tu wawaridhishe
wenzi wao au ili waonekane ni wanaume waliokamilika. Wanaume wengine
wamekuwa wakitumia dawa za kusimamisha mboo kama vile viagra au dawa za
asili na zingine maarufu kama dawa za kimasai! Napenda nikwambie kwamba
hizo dawa zina madhara makubwa kwa urijali wako na uko hatarini
kuupoteza hata huo urijali mdogo uliosalia!
Kusimamisha
mboo kwa muda mrefu na mara nyingine kiasi cha kufikia mboo inaanza
kuuma kutokana na kusimama muda mrefu tayari ni ugonjwa. Kwa maneno
rahisi ni kwamba umetumia dawa za kuongeza nguvu ili kuua nguvu chache
ulizokuwa nazo. Kitalaamu hali hiyo ya mboo kusimama muda mrefu na kuuma
inaitwa ‘Priapism’. Priapism hutokea pale mboo inapopoteza uwezo wake
wa kuondoa damu iliyoko kwenye mboo hiyo (ambayo hufanya isimame) ili
isinyae (in order to become flaccid). Hiyo hali ikidumu kwa muda wa
masaa manne husababisha seli za damu iliyoko kwenye mboo kukosa hewa ya
oksijeni, hivyo kupelekea tishu katika mboo kufa. Na kadri hali hiyo
inavyoendelea hupelekea damu kwenye mboo kuwa na asidi na hivyo kukosa
uwezo wa kusafiri au kutembea kwenda sehemu zingine za mwili hususan
kwenye moyo! Hapo hali inakuwa mbaya sana!
Kuna
wanaume wengine wanaji-overdose viagra au madawa ya kienyeji ili wawe
wanaume shababi kwelikweli kumbe ndio wanaua mboo zao. Ndio maana watu
wanaotumia madawa hayo baada ya muda fulani hali zao za kiume zinakuwa
mbaya zaidi afadhali ya jana! Ndio maana humu katika blog nimesisitiza
sana matumizi ya vyakula na viungo kama tiba ya tatizo la ngivu za
kiume! Siwashauri kutumia hayo madawa, otherwise, keep using them for
your own risk!
Bahati
mbaya au vyovyote vile kama umesimamisha mboo masaa kadhaa hakikisha
katika kipindi cha ndani ya masaa manne tafuta tiba haraka kwa daktari!
Wengine baada ya kutumia hayo madawa na mboo kusimama kama msumari masaa
mengi wao hudhani dawa ni kufanya mapenzi masaa mengi na mwanamke ili
kuondokana na hali hiyo! Tena wengine ndo hufurahia eti ‘leo mwanamke
fulani nitamfaidi kweli…’. My brother you are killing yourself’!!!
Hutoweza kumkomoa mwanamke kwa kufanya mapenzi! Matibabu ya tatizo hilo
ni kunyonya damu kwa kutumia sindano itakayochomwa kwenye mshipa wa damu
uitwayo vein kwenye mboo yako! Mwisho nakushauri kula sana vyakula vya
asili kama matunda na mboga za majani. Usisahau mazoezi ya viungo. Next
time tutaona namna ya kukabiliana na tatizo la nguvu za kiume ingawa
nimegusia gusia katika bloga hii katika mada kadhaa!
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments:
Post a Comment