Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.
1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo:
1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo:
Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila
wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya
moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya
endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na
hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara
tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo
(heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati
wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote
vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha,
sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa
na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo
vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea
kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa
kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza
na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi
mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.
2. Huongeza ukakamavu wa mifupa:
Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana
angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya
oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii
husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo
homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.
3. Hupunguza msongo wa mawazo:
Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya
mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za
dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle
relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi
mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri
msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu
wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko
wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vya prostaglandins katika
shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na
sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium,
potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.
4. Hupunguza maumivu:
Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni
ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na
viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso,
baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post
menopausal syndrome symptom).
5. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa
mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate
cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa
kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa
mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume
kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4
mpaka 7 kwa mwezi.
6. Huongeza uwezo wa kunusa:
Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo
hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika
sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb).
7. Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema:
Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo
huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na
mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200
calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill.
Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.
8. Huongeza kinga ya mwili:
Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha
seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga
mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke:
Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri
mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na
ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele
za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.
10. Kudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:
Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku
ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida
ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao
hawafanyi kabisa.
11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.
12. Kuongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): Na
hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha
mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa
mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection).
13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini:
Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu,
hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo
muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu
mbalimbali mwilini.
14. Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako:
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia,
haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza
wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza
hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.
15. Husaidia kuishi kwa muda mrefu:
Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila
unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa
kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza
kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda),
huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na
afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia
kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.
16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na
kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta
mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.
uongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama
urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri
ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume,
huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni
bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa
muda wa siku nne.
No comments:
Post a Comment