Kitu cha mwisho ambacho watu wanahitaji wakati wa mahojiano au migogoro ni katika kuingiza Upendo, joto la upendo.
Kuonyesha upendo ni kitu pekee ambacho kinafunika mambo yote wakati wa migogoro mbalimbali.
Kitu ambacho nimekigundua ni katika kukumbatiana, kumkumbatia
mwenza wako wakati mnapokuwa katika malumbano ya hoja yenu taratibu
inabadilisga hali yote ya machafuko. ukimkumbatia mwenza wako wakati wa
malumbano huwa inaleta hali tofauti, haiwezi kuwa kama siku zote
ambazo umezoea. imegundulika kuwa inakuwa na hisia za kweli, mtu anaweza
kujisikia vizuri zaidi kuliko ile kawaida ya siku zote, inaondoa hali
ya kuwa na shaka lolote.
Mtu yeyote anapokuwa na stress , kama akikumbatiwa vizuri na mtu ambaye ataweza kutumia muda wa kutosha kufanya hivyo, inamsaidia mhusika wa tatizo kuepuka kupata shinikizo la moyo
Nimegundua watu wengi wanapata tatizo la ugonjwa wa moyo na hata kufa
kwa sababu ya kukosa mtu maalum wa kumkumbatia anapokutana na
changamoto ya mahusiano, hasa katika malumbano mbali mbali .
Ukiona unapata shida kama hio na wakati huo labda mwenza wako amekuwa hajielewi vizuri , jaribu kutafuta mtu mwenye Upendo na Ile Huruma ya Mungu. Yaani Love and compassion.
Love and compassion ni zawadi kutoka kwa Mungu, ni Neema fulani hivi mtu anapewa na Mungu, Ukikutana na mtu kama huyo , hata kama ulikuwa na maumivu ya aina gani , utajikuta unapona saa ile ile kwa ajili ya mguso ambao utapata kutoka kwake.
Ni kama vile umeme unaingia kwa mtu haraka na kuponya kila kitu.
Kwa hio kumkumbatia mtu sio tu suala la kimwili, bali ni katika kuponya nafsi ya mtu.kwa sababu magonjwa yote yanaanzia kwenye akili, magomvi yote yanaanzia kwenye akili ya mtu.
Pia kukumbatiana kunaleta ukaribu , uaminifu, na kuleta ufahamu wa
kikomavu ambao ni wa kujali mtu, inaleta upendo wa kipekee, kujiamini,
urafiki na kuweza kufahamu silika ya mtu ambayo itakusaidia
kuwakumbatia watoto wetu, wazazi wetu na marafiki zetu.
wapo watu tangu wamekua na akili, hawajawahi kuwakumbatia wazazi wao, pia kuna watu ambao hawana tabia ya kuwakumbatia watoto wao. Hili ni tatizo kubwa ambalo nimeligundua mimi binafsi kuwa ipo haja kubwa ya kukumbatiana kila inapobidi, iwe ni mtoto , au mzazi au rafiki , hasa ukiona yupo katika hali ambayo sio ya kawaida. Jitahidi kufanya hivyo utaona unamponya mtu kwa namna ya kipekee.
Hug inaweza isiwe suluhisho la mara moja wakati wa tatizo, lakini kama ukifanyia zoezi inaweza kusawazisha hali mbaya kuwa nzuri.
Kuonyesha upendo ni kitu pekee ambacho kinafunika mambo yote wakati wa migogoro mbalimbali.
Mtu yeyote anapokuwa na stress , kama akikumbatiwa vizuri na mtu ambaye ataweza kutumia muda wa kutosha kufanya hivyo, inamsaidia mhusika wa tatizo kuepuka kupata shinikizo la moyo
Ukiona unapata shida kama hio na wakati huo labda mwenza wako amekuwa hajielewi vizuri , jaribu kutafuta mtu mwenye Upendo na Ile Huruma ya Mungu. Yaani Love and compassion.
Love and compassion ni zawadi kutoka kwa Mungu, ni Neema fulani hivi mtu anapewa na Mungu, Ukikutana na mtu kama huyo , hata kama ulikuwa na maumivu ya aina gani , utajikuta unapona saa ile ile kwa ajili ya mguso ambao utapata kutoka kwake.
Ni kama vile umeme unaingia kwa mtu haraka na kuponya kila kitu.
Kwa hio kumkumbatia mtu sio tu suala la kimwili, bali ni katika kuponya nafsi ya mtu.kwa sababu magonjwa yote yanaanzia kwenye akili, magomvi yote yanaanzia kwenye akili ya mtu.
wapo watu tangu wamekua na akili, hawajawahi kuwakumbatia wazazi wao, pia kuna watu ambao hawana tabia ya kuwakumbatia watoto wao. Hili ni tatizo kubwa ambalo nimeligundua mimi binafsi kuwa ipo haja kubwa ya kukumbatiana kila inapobidi, iwe ni mtoto , au mzazi au rafiki , hasa ukiona yupo katika hali ambayo sio ya kawaida. Jitahidi kufanya hivyo utaona unamponya mtu kwa namna ya kipekee.
Hug inaweza isiwe suluhisho la mara moja wakati wa tatizo, lakini kama ukifanyia zoezi inaweza kusawazisha hali mbaya kuwa nzuri.
No comments:
Post a Comment