Ingawa
kuna mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa ukishamuoa mwanamke na mkawa
mwili mmoja basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa
wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.
Lakini
utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa
waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na
waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume
wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero
au kuwakwaza wake zao.
Kama
tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu
kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu
wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu
ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie
sana anataka kukidhi haja yake.
Ukifuatilia
sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake,
utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo
anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa.
1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani
Idadi
kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati
wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama
mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi
maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko
‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo.
2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga
Wanaume
wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake
zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi.
Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka
mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na
kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati
ambapo wametokwa jasho.
3. Sehemu za siri kabla ya kuoga
Hili
ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa
mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa
pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi
wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa
na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.
Wanaume
wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya
kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza
kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba
hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa
amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo
wanajiamini ni wasafi.
4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba
Ingawa
unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia
wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya
kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia
ulimpa wewe.
Hiki
ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu
sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili
waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa
saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema
mtaharibiana ‘mood’.
Haya
ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na
kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati
ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments:
Post a Comment