Kukosa
hamu ya kujamiiana ni tatizo linalowasumbua wengi nchini. Ni maradhi
kwa upande mwingine yanayosababisha ugumba na hata mifarakano na
kuvunjika kwa ndoa.
Masanja
na mke wake Saumu wameishi kwenye ndoa kwa miaka kumi sasa. Hapo awali,
kila kitu kilikuwa sawa katika uhusiano wao, lakini katika miaka ya
karibuni, Masanja amekuwa hana matamanio tena na Saumu; hana hamu kabisa
ya tendo la ndoa.
Tatizo
hili limekuwa likiwaathiri watu wengi hapa nchini na hata duniani kote.
Haliwaathiri wanaume pekee kama ilivyo kwa Masanja, bali hata wanawake
nao hukumbwa na tatizo hilo.
Utafiti
uliofanyika nchini Uingereza , Ulaya na Marekani, ukijumuisha wanawake
wa rika zote, ulibaini kuwa asilimia kati ya 30 na 50 ya wanawake
wanakumbwa na tatizo la kukosa hamu ya kujamiiana.
Wakati
huo utafiti huo ukiweka bayana hilo kutokana na tatizo la uzazi au
kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya
wanawake hawafikii kilele cha tendo hilo au wanapata maumivu.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kukosa hamu ya tendo la ndoa kunatibika, iwapo hatua muhimu na za msingi zitachukuliwa.
Ni vyema kufika mapema katika huduma za afya ukiwa na mwenza wako kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Nini suluhisho la kukosa hamu ya kujamiiana
Kwanza
kabisa, inashauriwa kitaalamu kubadilisha mfumo wa maisha kwa mfano,
kubadili ratiba za kazi, matembezi au ratiba za wenza.
Kingine
ni kufanya mazoezi mara kwa mara kwa sababu mazoezi huongeza ufanisi,
lakini pia kupunguza uzito na humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha
na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiiana.
Kupunguza
msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na
hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha
lazima yatafutiwe ufumbuzi.
Kufanya
mazoezi ya misuli ya kiuno kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati
unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano
pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa
kujamiiana kwa wanawake
Kubadilisha mfumo wa maisha kwa wapenzi
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Tiba ya vichocheo (homoni)
Mdalasini na Asali– Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili.
Zungumza
na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika
uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo
yao, kuwa wa kweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu
ya tendo la ndoa kwa pamoja.
Ni
vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa
wakati wa kujamiiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishwa
na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi hana budi kutumia lugha nzuri
kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu.
Ongeza
msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali
wakati wa kujamiiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu
hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile mliyoizoea wakati wa
kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani).
Kupata
ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, ndoa na hata
madaktari wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi
yao.
Tiba ya dawa
Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk.
Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazosababisha madhara kama ya msongo wa mawazo na sonona.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Kutumia dawa au vilainishi vya ukeni wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza uke kuwa mkavu au kuwasha.
Tiba ya vichocheo (homoni)
Dawa
za kitaalamu za kuongeza hamu au nguvu atakuandikia daktari baada ya
kufahamu kiini cha tatizo. Haishauriwi kutumia bila ushauri wa daktari
kwani dawa hizi zina madhara.
Ikumbukwe
ya kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia tu kupunguza
ukubwa wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya kujamiiana na
kuboresha kwa wale ambao hawana tatizo hili na hivyo kudumisha uhusiano.
Kitunguu
swaumu – Kitunguu swaumu kina kemikali ambayo huongeza mzunguko wa damu
kwenda kwenye uume, huongeza hamu ya kufanya mapenzi na utolewaji wa
mbegu za kiume.
Habat
al soda – Mafuta, mbegu, au unga wa habat soda kama wengi wanavyoiita
na ambazo zimetumika kwa miaka mingi sana kupunguza tatizo hili na
waandishi wengi wa tiba ya nguvu za kiume wameeleza umuhimu wake. Tumia
kidogo kwenye chai au maji ya uvuguvugu mara mbili kila siku. Mbegu
hizi hupatikana kwa wingi katika nchi za asia kama Saudi Arabia, Syria,
Iran, Dubai (UAE), na hata Misri, Tanzania-maeneo ya pwani hupatikana.
Giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.
Ndizi
– kuwepo kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya ‘bromelain’ na madini ya
potashiam, huongeza msisimko wa tendo kwa wanaume. Potassium pia
hupatikana kwenye tikiti maji ambalo pia lina kemikali aina ya
‘arginine’ ambayo huongeza wingi wa damu katika mishipa ya damu na
hivyo kusaidia katika kusimika kwa uume.
Parachichi
– Huwa na kiwango kikubwa cha madini ya folic acid ambayo huvunjavunja
protini. Vitamini B6 kwenye parachichi huchochea kutengeza vichocheo
vya kiume kwa wingi.
Mayai
– Mayai yana kiwango kikubwa sana cha vitamini aina ya B5 na B6, ambazo
husaidia kuleta usawa wa viwango vya vichocheo mwilini na kupunguza
msongo wa mawazo.
Nyanya
– Zina kiwango kikubwa cha virutubisho aina ya bio-active
phyto-nutrients, lycopene, na beta carotene ambazo husaidia kuleta damu
kwa wingi kwenye uume na hivyo kusaidia kusimika kwa uume
‘Chocolate’ – Ina kiwango kikubwa cha kemikali ambazo huongeza hamu ya tendo.
Vitamin
A – Husaidia katika kuweka usawa wa vichocheo vya mapenzi. Vyakula
venye wingi wa vitamin hii ni pamoja na karoti, maini,tikiti maji,
spinach, maziwa nk.
Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone ambacho
husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume na
wanawake. Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi
tamu, lentils mboga za majani, parachichi, mayai, samaki aina ya jodari
(tuna), bata mzinga, maini nk.
Mdalasini na Asali– Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments:
Post a Comment