Hello reader wa Nesi Mapenzi! Somo la leo ukimaliza kulisoma nataka
ukajaribu angalau mara moja. Najua kuna baadhi ya watu ambao washawahi
hujaribu na kufaulu (kawaida unafaulu asilimia 100 kila wakati), so somo
lenyewe ni kuapproach mwanamke katika gari la usafiri la abiria.
NB Wakati mnapowasiliana, hakikisha mazungumzo yenu hayavunjiki.
Kuna abiria wengine huongea dakika mbili tu halafu kule kwingine wanaua
mazungumzo, haupaswi kufanya hivyo. Hakikisha pia katikati ya mazungumzo
yenu unachukua namba yake ya simu. Halafu wale wanaopenda kufanya
vituko wakiwa safarini unaweza kutumia ile mbinu yetu ya kuwasisimua
wanawake.
Ok, hebu tuanze hivi, ni mara ngapi ushawahi kuingia katika basi
ukakutana na mwanamke mrembo ukamtamani? Ama ni mara ngapi ukiwa ndani
ya gari ushawahi kumwona mwanamke mrembo ameingia na kukaa mbele yako?
Ni mara nyingi. Mambo kama haya hutokezea kila siku. Mwanzo kila siku
unapoabiri basi huwa unakutana na wanawake tofauti tofauti na warembo.
Na je, unajua mbinu ya kuwaaproach uanze mazungumzo? Somo letu
litafafanua kwa upana.
Wanawake wakiwa ndani ya magari ya usafiri huwa rahisi kuwaaproach
tofauti na sehemu nyingine unazozijua. Hii ni kwa sababu ya mambo haya:
1. Kinga zake ameziweka chini. Katika gari za usafiri mwanamke
huwa hayuko katika hali ya kutangamana, so hatakuwa na mawazo katika
akili yake kama vile anavyokuwa katika kilabu. Mfano hafikirii mbinu za
kukabiliana na wanaume wanaoudhi ama kuwa na wasiwasi wa kwanini hakuna
mtu mpaka sahizi amemuaproach. Nguvu zake zote katika gari la usafiri
huwa zimetulia ukilinganisha na wakati ameenda kula bata na marafiki
zake usiku. Katika hali hii huwa ni rahisi kumuaproach na anaweza
kuungana na wewe kirahisi bila matatizo.
2. Gemu huwa ya juu. Katika magari ya usafiri wanawake ni wengi
mno. Kila siku ukisafiri utakutana na wanawake tofauti. Wale ambao
utakutana nao leo, si wale ambao utakutana nao kesho. Hii inamaanisha
kuwa kadri utakapokuwa ukisafiri ndipo utakapokuwa na nafasi nzuri ya
kuchagua mwanamke unayetaka wewe.
3. Una mstari ambao unafanya kazi kila wakati. Kuanza mazungumzo
na mwanamke ni rahisi katika magari ya usafiri. Sentensi kama,
"Unasafiri ukielekea wapi?" Tayari inaweza kuamsha mazungumzo yasiyokuwa
na mwisho.
Ok. Hapo juu tumeonyesha sababu muhimu ambazo zinafanya kuapproach mwanamke katika gari la usafiri kuwa rahisi kuliko zote.
Kuna aina tatu za kumtambua mwanamke abiria. Nazo ni kama zifuatazo:
Hali #1 Mumesimama nje ya gari la usafiri unangojea kuingia ndani ukamwona mwanamke unayempenda. Katika
hali hii mara nyingi hutokea katika basi. Abiria wote wako nje
wanangojea kuabiri basi, halafu ghafla ukakutana na mwanamke
unayevutiwa. Hatua ya kufanya hapa ni rahisi. Unachotakiwa kuanza ni
kwenda hadi pale alipo, simama karibu yake halafu umwambie, "Waah, leo
abiria ni wengi/wachache. Hivi unaelekea wapi?" Hapa atakujibu bila
wasiwasi wowote sababu kinga zake zote ameziweka chini (sababu tumeeleza
hapo juu).
Akikujibu usimalizie hapo, mwambie pia wewe unaelekea wapi. Katika
mazungumzo yenu hakikisha unaongea mada ambazo zinazungumzia usafiri,
usiingize siasa wala michezo. Halafu kuaproach hivi lazima uwe mtu
asiyemwoga. Kama unatatizika na uoga wa kutojiamini ingia hapa. [Soma: Jinsi ya kuondoa uoga wa kuaproach mwanamke]
Sasa mazungumzo yenu hayaishi hapo nje, lazima uingie ndani ya gari.
Sasa hapa kuna changamoto kidogo. Kama unaingia ndani ya gari ambalo
kiti unajichagulia mwenyewe utakuwa umefaulu kumnasa. Kama tayari
mumepewa tiketi ambayo kila mtu ameandikiwa kiti chake itakuwa vigumu
kuendelea na appraoch kwa huyu mwanamke kama kiti chako ni nambari 12 na
yeye ni 35.
Turudi kwa kujichagulia kiti mwenyewe; Wakati mnapoingia kwa basi,
unamwambia maneno kama, "Mi hupenda kuketi katika viti ya katikati,
ingekuwa bora tukae katika viti vya nambari 23 na 24." Ukimwambia maneno
kama haya hawezi kupinga. Mwanzo ushajitokeza kama mwanaume alpha,
jambo ambalo wanawake wanapenda.
Ama unaweza kutumia mbinu nyingine nzuri ya kumwonyesha sehemu ya kuketi
kwa kutumia ishara. Mfano wakati mnaingia ndani ya basi, elekeza sehemu
unayotaka akae, mwambie, "kaa hapa sehemu ya dirisha." Akishaketi sasa
wewe unafuatilia. Hii ni mbinu nyingine rahisi ya kufuatilia.
Kwa kuwa tayari mazungumzo yenu yalianza mkiwa nje ya gari, ni rahisi kuendelea hadi umwombe namba yake ya simu. [Soma: Mbinu za kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke]
Hali #2 Unaingia ndani ya gari la abiria halafu unamwona mwanamke amekaa pembeni akiwa pekeake. Hapa moja kwa moja unaenda kukaa sehemu alipo. Anza na mstari wa, "Unaelekea sehemu gani?" halafu mazungumzo yaanze na hapo.
Hali #3 Umekaa nyuma ya gari, ghafla mwanamke mrembo akaingia na kukaa viti vya mbele pekeake. Hatua
kama hii unapaswa kuwa mjanja. Jambo la kufanya ni kuhakikisha kuwa
mwanamke aina hii hakukuona. Hakikisha hajaona sura yako. Akishaenda
kukaa kwa kiti sasa unaweza kubeba ujasiri wako na kuaproach sehemu
alipo. Hapa lazima ufahamu mambo mawili. Kwanza ni kuwa ukienda kukaa
sehemu yake lazima atajua kuwa ulikuwa ndani ya gari so lazima uwe na
sababu za kwa nini umeenda kukaa na yeye. Pili ni kuwa usipojieleza
ukaeleweka unaweza kumfanya mwanamke kama huyu kuziamsha kinga zake
hivyo ukakosa kila kitu. So hivi ndivyo unavyopaswa kusema wakati umekaa
na yeye, "Kule nyuma kuna joto na unarushwarushwa kila wakati, nimekuja
hapa mbele angalau nafeel kibaridi na hewa safi." ama "Nimekuona
ukiingia kwa hili gari nikaona si vizuri kumwacha mwanamke nadhifu kama
wewe ukae pekeako, waendeleaje lakini?"
So, je kama mimi sina kitu cha kuongea? Kama hujui utasema nini basi
hupaswi kuapproach mwanamke aina hii mpaka ujue jinsi ya kuwazoea
wanawake. [Soma: jinsi ya kujifunza kuongea na wanawake].
Mazungumzo ukiwa katika gari la abiria ni rahisi sana. Mwanzo
unazungumzia kuhusu gari lenyewe na kampuni inayomiliki, unazungumza
kila kitu kuanza mwenendo hadi mwishio, unaongea kuhusu sehemu unayoenda
na uliyotoka, vitu mnavyokumbana navyo barabarani nk, yaani mazungumzo
hayana mwisho.
No comments:
Post a Comment