Ni ndoto ya kila mwanamume kuwa bingwa kitandani lakini nyakati
zingine ngoma hukosa hata kushika kasi, na kuwafanya wanaume hao
kukandamizwa na mawazo
– Watafiti, hata hivyo, wamebaini vyakula fulani ambavyo wanakushauri kuvitumia kuimarisha ngoma
1. Kahawa
Kikombe cha chai ya kahawa huwa na kafeini ambayo huimarisha
metaboli ya mwili. Vile vile, hufanya moyo kudunda haraka na kwa nguvu
na hivyo kusambaza damu kwa kasi mwilini, hadi kwa mzinga. Haya ni mambo
muhimu kwa mwanamume kushiriki mapenzi vilivyo.
Utafiti unaonyesha kuwa kafeini pia humpa mwanamume uwezo wa kudumu
kileleni, na hivyo kumwezesha kuhifadhi nguvu za kutumia wakati ngoma
inahitaji nguvu mpya.
2. Soseji
Ni muhimu kwa neva za mzinga kuwa ngangari ili kukupa uwezo wa kufanya shughuli kitandani.
Utahitaji kula vyakula vya Vitamini B1, ambazo hupatikana katika
soseji ya nguruwe. Iwapo hupendi kula soseji, pata vitamini hizo kwa
maharagwe ama mkate ulioundwa kutokana na unga ambao haujakobolewa.
3. Divai
Divai ni kinywaji tosha kuimarisha nguvu za kiume, hususan divai
nyekundu. Hii imebainika kutoa virutubishi vya kemikali ya nitric oxide
ambayo husaidia kupanua mishipa mikuu ya damu na kuimarisha mtiririko
hadi kwa mzinga.
Kemikali hiyo hufanya kazi kama tu Viagra – kupanua kabisa mishipa
mikuu ya damu – ingawa tofauti ni kuwa vidonge hivyo husababisha mishipa
hata midogo katika eneo la uume kupanuka.
Tahadhari: usinywe glasi nyingi kwani itakuletea madhara.
4. Uji
Uji huchukuliwa kama kinywaji cha watoto, lakini uji uliotengenezwa
kutokana na unga ambao haujakobolewa huwa na nyuzi zinazosaidia kuondoa
kolestorol kwenye damu.
Damu ikiwa sawa mtiririko ni haraka na mishipa inaweza kustahimili
kishindo kinachotokana na shughuli nzima ya ngoma. Iwapo unataka mzinga
kusimama wima kileleni, kopo la uji litakufaa!
5. Ndizi
Ndizi hukupa Vitamini B inayokuwezesha kuhifadhi nguvu za kimwili
na kukuondolea mawazo. Vile vile, zimejaa homoni za serotonin na
potasiamu ambazo zinatumika kuunda homoni za mahaba na ile ya bromelain,
ambayo ni aina ya kemikali inayoimarisha mtiririko wa damu mwilini.
No comments:
Post a Comment