Unaweza kuwa na girlfriend kwa muda mrefu na usiweze kujua kama
anakupenda au la. Wanawake wengine wanaweza kujifanya girlfriend wazuri
kumbe wanakutumia. Na pia unaweza kuwa na girlfriend halisi ambaye
anakupenda kuanzia juu mpaka chini.
Hapa Nesi Mapenzi leo tumekuletea ishara zote ambazo zitakuonyesha iwapo mwanamke/girlfriend wako anakupenda au la. Zama nasi.
Ishara kuonyesha kama mwanamke/girlfriend wako anakupenda.
#1 Anakufanyia yale mambo madogo madogo kuyafanya maisha yako kuwa rahisi. Kama
mwanamke anakupenda basi jambo la kwanza la kufanya ni kuonyesha upendo
kwa anayempenda. Kama unamwona anakukunjia nguo zako, anakutembelea
kuhakikisha nyumba yako iko safi ama kuhakikisha hausahau kununua kitu
muhimu kwa nyumba yako basi ujue anakupenda.
#2 Anakuoshea nguo. Kama anakufanyia kitu nyumbani kwako ambacho
yeye mwenyewe huwa hapendi kufanya kwake basi ni ishara nzuri. Anajaribu
kuonyesha uanawake wake kinyumba. Katika DNA ya mwanamke ni kuwa
ameumbwa kuwajali wale ambao anawapenda ili kuwarahisia maisha. Kama
girlfriend wako anaonyesha hizi tabia basi ujue anakupenda.
#3 Kando na kuwa anajua chakula unachokipenda, anajaribu kukitengeneza. Anajua chakula nachokipenda? Ashawahi kukutengezea mara kwa mara? Huyo anakuonyesha kuwa anakupenda.
#4 Anaelewana na familia na marafiki zako hata kama hawamthamini. Kama
girlfriend wako anatabasamu hata kama familia yako inachukiza, basi huo
ni upendo. Kwa kawaida wanawake hawaelewani na familia ya mwanaume.
Lakini ukiona anajaribu bila kulalamika, hio ni ishara ya upendo kwako.
#5 Anakatiza shughli zake kuja kukuona. Kama yuko tayari kuuza
tiketi yake ya kwenda kwa concert ya Diamond ili aspend usiku na wewe,
hio ni ishara ya kukuambia, "nakupenda."
#6 Anayaweka matakwa yako mbele. Ukiona yuko tayari kufunja
sherehe na marafiki zake ili asherehekee na familia yako ama kwenda kula
dinner na marafiki zako ni ishara ya mapenzi.
#7 Anakusifia pale ambapo inahitajika. Mwanamke ambaye anakupenda
hataona tatizo kukusifia pale ambapo kunahitajika. Kuambia mtu kuwa
unampenda kunaonyesha kuwa unamthamini.
#8 Ni mtu wa kwanza kukupigia iwapo ana furaha, huzuni ama hasira. Kitu
chochote ambacho kitamtokea yeye atakuwa wa kwanza kukuambia. Hii
inamaanisha anakupenda na anakuamini. Uwepo wako kwake anaudhamini na
kuuzingatia.
#9 Atakwambia mambo ambayo hayapenda. Ashawahi kukuambia mambo
yaliyomuaibisha, huzunisha ama kumfelisha? Ukiona anakwambia kila kitu
hata siri zake za kuzimu basi fahamu kuwa anakupenda.
#10 Anaonyesha ukichaa wake. Hakuna mtu anaweza kufunguka
asilimia 100 tabia zake kwa yeyote. Ukiona amekuwa huru na wewe kiasi
cha kuwa anaweza kuachilia hewa, kukuonyesha sura za kiajabu, ama
kufanya mambo ambayo hukutarajia, basi ni ishara ya kuwa penzi lake
kwako ni la dhati.
#11 Anashikwa na wivu ukiongea kuhusu wanawake wengine, lakini si sana. Mwanamke anayekupenda huwa hapendi kuskia ukiwasifu wanawake wengine. Hio ni kawaida.
Hizi ni baadhi ya dalili kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda. Je
girlfriend wako anaonyesha hizi tabia ama ni mtofauti na tabia hizi
tulizozitaja? Uamuzi ni wako sasa.
No comments:
Post a Comment