Ndoa au mahusiano mengi huvunjika na sababu kuu ikiwa ni waliochumbiana
au waliooana baada ya kuishi kwa muda kutambua kuwa wapenzi wao hawana
faida katika maisha yao. Hapa Nesi Mapenzi tumekuja na suluhisho hili
angalau utambue je huyu unayechumbiana naye amekamilika ama anabahatisha
tu.
Zifuatazo ni ishara za kumtambua iwapo mpenzi wako ni perfect.
Zifuatazo ni ishara za kumtambua iwapo mpenzi wako ni perfect.
#1 Mpenzi wako ni msiri. Katika mapenzi mara nyingi siri lazima
iwepo kati ya wapenzi wawili. Kuna wapenzi wengine hawajui kuweka siri.
Waeza kupata mwanaume ana lalamika kwa Rafiki zake kuwa mpenzi wake si
bora kitandani. Jambo kama hili lafaa liwe siri kati yenu. Njia bora ni
kukaa nay echini umfunze jinsi gani anaweza kuwa Hodari kitandani badala
ya kumuanika na kumsema kwa marafiki zako.
#2 Mpenzi wako hukusaidia. Hapa ndipo penyewe sasa. Katika
mapenzi maisha huwa ni kusaidiana. Iwapo mpenzi wako hatoi msaada wowote
huyo achana naye. SI msaada wa pesa pekeake bali hata pia msaada wa
kimawazo unatakikana katika mapenzi. Tena wapenzi hawafai kuwa mkono
nirika. Eeehe! Mpe mpenzi wako zawadi, mtoe dating, mfanyie surprise.
Hayo ndio mapenzi.
#3 Mpenzi wako hukutakia mema. Hahahah! Nyie mlio wapenzi je
huombeana mema? Si eti wamtakia mpenzi wako mabaya ili umuadhibu. Eti
nimemuomba mwanaume wangu pesa akakataa Mungu amjalie agongwe na gari
ndio hizo pesa zitumike hospitali tukose wote. Wewe mwanamke ushindwe.
Hata kama umenyimwa pesa usimwombee mpenzi wako mabaya kwani hujui pesa
alizo nazo zina hesabu gani.
#4 Anatatua ugomvi kivipi. Je mpenzi wako hutumia njia zipi ili
ugomvi wenu usifike mbali? Kuna wapenzi ambao huona njia bora ya
kusuluhisha ugomvi ni kunyamaziana kwa muda. Hapana. Hii njia huvunja
mahusiano kabisa. Njia bora ni kukaa chini muangalie tofauti zenu halafu
msuluhishe tatizo lenu wenyewe.
#5 Anakukubali jinsi ulivyo. Enyi wapenzi inapaswa ukubali
unyonge wa mpenzi wako na kama ikiwezekana msaidie kwa kumrekebisha.
Kunao wanaopendana lakini mmoja kati yao huwa na hasira za haraka,
kulalamika bila mpango nk. Matatizo kama haya ni magumu kuyarekebisha.
Hivyo basi unapaswa umkubali na ushughulikie tatizo lake polepole na
wala usimkemee.
#6 Anakuheshimu. Heshima ni muhimu katika mahusiano. Mahusiano
bila hishama hapo hakuna upendo wala mapenzi. Heshimianeni ndio muikuze
heshima yenu mpaka ule wakati mtachumbiana. Kama mpenzi wako hakuheshimu
basi huyo hakufai. Mtu kama huyo atakuwa nuksi tupu katika maisha yako.
#7 Anakushauri. Utamu wa mapenzi ni kushauriana na wala si
kufokeana. Ni vyema mpenzi wako akikukosea akushauri badala ya
kukufokea. Hii ni tabia ya wazimu. Dadangu na kakangu usikubali kabisa
mpenzi wako akufokee badala yake anapaswa kukushauri. Ushauri wenyewe
unapaswa kuwa mwema na wala si mbaya.
No comments:
Post a Comment